Kuomba kupata Mafunzo, Tukio la Uhamasishaji au Kliniki ya Jamii

Kuomba kupata Mafunzo, Tukio la Uhamasishaji au Kliniki ya Jamii

Tunaboresha hali ya kuelewa ya jamii na familia kuhusu jinsi shule zetu za umma za K-12 zinavyofanya kazi ili shule, familia na jamii ziweze kuanzia katika sehemu moja ili kufanya maamuzi yanayowasaidia wanafunzi, kuimarisha uhusiano baina ya familia na shule na kupunguza mapengo ya fursa.

Tunatoa maonyesho, mafunzo na uhamasishaji usiolipishwa kuhusu aina mbalimbali za masuala! Pia tunatoa kliniki za jamii kwa ushirikiano na mashirika yasiyo ya faida au shule ili kuleta huduma zetu za wapelelezi wa malalamiko ya wananchi (ombuds) moja kwa moja katika mtaa wako panapowezekana.

Baadhi ya mafunzo yetu ya hivi majuzi yameshughulikia usuluhishaji wa migogoro; ushirikishaji wa familia; unyanyasaji, vitisho na ukandamizaji (HIB); nidhamu shuleni; usaidizi kwa wasio na makao au vijana wanaopata malezi ya kambo; ufikiaji wa huduma za lugha; na huduma kwa wanafunzi walio na ulemavu. Tunazingatia zaidi kujenga uwezo wa jamii ili kupanua eneo la huduma la wafanyakazi wetu wachache. Ikiwa una habari nzuri, unaweza kusaidia wanafunzi wengi kufaulu!

OEO inaweza kufanya mafunzo yafae zaidi kwa familia, vikundi vya jamii, viongozi na waelimishaji ili kutimiza mahitaji yao. Tumeorodhesha hapa chini sampuli chache za maelezo ya jumla kuhusu mafunzo ya OEO ili kukupa ufahamu wa huduma zetu.

Chini ya mpango wetu wa kimkakati, tunapanua lengo letu la mafunzo na matukio hadi mwaka wa 2023 yanayoshughulikia wanafunzi wa K-12 ambao:

  • Hawaendi shuleni, ikiwa ni pamoja na wanafunzi walio na ulemavu ambao hawapokea huduma ya masomo kwa siku nzima
  • Ni watu wasio wazungu, Waafrika au wa makabila ya asili 
  • Hawana makao
  • Wanaopata malezi ya kambo au wanaoishi na jamaa zao 
  • Wamechukulia hatua ya kisheria ya uhalifu wa vijana au walio katika mifumo ya kurekebisha tabia za vijana
  • Ni wahamiaji rasmi au wasio rasmi, wakimbizi, watafutaji makazi rasmi au wanafunzi au familia ambazo lugha zao za msingi si Kiingereza au
  • Wanapokea usaidizi wa Vipengele Mbalimbali vya Huduma za Kina (Wraparound with Intensive Services (WISe)) au usaidizi wa Mipango ya Watoto ya Wagonjwa Wanaolazwa kwa Muda Mrefu (Children’s Long Term Inpatient Programs (CLIP))

OEO ina wafanyakazi na nyenzo chache za kusafiri na inayapa kipaumbele matukio ambayo yanafikia:

  • Hadhira kubwa
  • Matatizo ambayo yanapatikana katika mpango wetu wa kimkakati na yanayoongeza usawa wa kielimu
  • Kujenga uwezo wa jamii kupitia muundo wa ‘wafunze wakufunzi’
  • Maonyesho yanayoweza kuwasilishwa mtandaoni, kama vile mikutano ya mtandaoni inayoshirikisha

Timu yetu imejitolea kutoa haki kwa walemavu na uwezo wa walemavu kufikia huduma za lugha.

Ikiwa ungependa timu yetu kufanya onyesho kwenye tukio lako lijalo, tunaomba kuwa uchukue hatua zifuatazo kama mpangishaji wa tukio ili kuunga mkono jitihada zetu hizi za ujumuishaji:

  • Tengeneza vipeperushi vinavyoweza kufikiwa au nyenzo zingine za kutangaza tukio na mtu wa kuwasiliana naye kwa ajili ya kupata huduma za lugha na ufikiaji wa walemavu na malazi
  • Jitolee kutoa malazi na ufikiaji huo
  • Pangisha tukio katika eneo linaloweza kufikiwa
  • Toa vipaza sauti (k.m, maikrofoni, spika) kwa washiriki

Kwa upande wetu kama mshirika wako,:

  • Tutahakikisha kuwa shughuli na nyenzo zetu za maonyesho zinaweza kufikiwa
  • Tutakusaidia kupata maelezo zaidi kuhusu ufikiaji na utambuzi wa nyenzo

Tunasubiri kwa hamu kushirikiana nawe!

Sehemu moja ya kuanzia kwa ajili ya kufanikisha mchakato wako wa kufikiwa ni Mwongozo wetu kuhusu Mipango ya Matukio Yanayoweza Kufikiwa. Utapata masharti kuhusu kuboresha ufikiaji wa matukio yako hapa.

Ikiwa ungependa kuandaa onyesho, mafunzo, tukio la uhamasishaji au kliniki, tafadhali wasiliana na oeoinfo@gov.wa.gov ili uulize kuhusu upatikanaji.