Kutuhusu

Mwaka wa 2006, Bunge la Jimbo la Washington lilipitisha Mswada wa Bunge 3127 wa kuanzisha Ofisi ya Wapelelezi wa Malalamiko ya Wananchi kuhusu Elimu (Office of the Education Ombuds (OEO)) ili kupunguza pengo la fursa kwa kusaidia familia, wanafunzi, waelimishaji na jamii kuelewa mfumo wa elimu ya umma wa K-12 na kutatua matatizo kwa ushirikiano. Bunge lilitutengea nafasi katika Ofisi ya Gavana ili kuhakikisha uhuru wetu kwenye mfumo wa elimu ya umma.

Tuna nyenzo chache na tunaupa kipaumbele usaidizi wetu wa moja kwa moja wa Upelelezi wa Malalamiko ya Wananchi (Ombuds) kwa masuala yanayopatikana katika mpango wetu wa kimkakati na ambapo tunaweza kuwa na athari nzuri kama watatuzi wa matatizo kwa ushirikiano kuhusu hali ya mwanafunzi. OEO inafanya kazi kote jimboni na idadi ndogo ya wafanyakazi wa wakati wote wasiozidi 7.

MAJUKUMU YETU

  • Kusikiliza matatizo na kushughulikia maswali kuhusu mfumo wa elimu ya umma wa K-12
  • Kutumia zana ambazo si rasmi za utatuzi wa migogoro ili kuwezesha usuluhishaji wa matatizo kwa pamoja na kuendeleza haki ya kielimu
  • Kutoa ukufunzi, uwezeshaji na mafunzo kuhusu ushirikishaji wa familia na jamii na utetezi wa mifumo
  • Kukusanya data na kutambua mitindo itakayotuwezesha kutoa mapendekezo ya sera za elimu