Pata Usaidizi Wetu

Pata Usaidizi Wetu:

Black and White Icon of electronic device sending message. Created by Priyanka from Noun Project Mtandaoni – Tunakuhimiza utumie Mchakato wetu mpya wa Kujiandikisha Mtandaoni. Utahitaji kufungua akaunti kwa kutumia jina lako na anwani sahihi ya barua pepe. Baada ya kufungua akaunti na kukamilisha mchakato wa kujiandikisha mtandaoni, mtu fulani atawasiliana nawe haraka iwezekanavyo ili kukupa maelezo au kuratibu miadi. Mchakato wetu wa kujiandikisha mtandaoni unapatikana kila wakati, lakini mtu fulani atafuatilia wakati wa saa za kawaida za kazi.

Saa za Kazi

  • Jumatatu saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni (8:00 a.m. – 6:00 p.m.)

  • Jumanne saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni (8:00 a.m. – 4:00 p.m.)

  • Jumatano saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni (8:00 a.m. – 4:00 p.m.)

  • Alhamisi saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni (8:00 a.m. – 6:00 p.m.)

  • Ijumaa saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni (8:00 a.m. – 6:00 p.m.)

Calendar by ghufronagustian from NounProject.com

Ratibu Miadi ya Kuchukua - Panga muda kwa mtaalamu wa ulaji kukupigia simu, kukusanya taarifa muhimu, na kushauriana nawe kuhusu swali au hali yako. Vinginevyo, unaweza kukamilisha taarifa zinazohitajika kwa urahisi wako kwa kutumia Mchakato wa Uingizaji wa Mtandaoni.

Black and white icon of mobile phone making a call. Created by Thays Malcher from Noun Project.Kwa Simu – Ikiwa unapendelea kuzungumza na mtu ana kwa ana au unahitaji usaidizi wa kukamilisha mchakato wa kujiandikisha mtandaoni, tafadhali tupigie simu kwa nambari ya simu isiyolipishwa 1-866-297-2597 wakati wa saa zetu za kazi za Jumatatu hadi Ijumaa. Wafanyakazi wetu wanaweza kufikia huduma za ukalimani wa simu kwa zaidi ya lugha 150.

Black and white icon of envelope with two papers inside. The first paper has the "at" email icon. The second paper has lines for writing a letter. Created by Anang Taufik from Noun Project.Kwa Faksi au kwa Barua – Pakua fomu ya Kuomba Huduma za Wapelelezi wa Malalamiko ya Wananchi (Ombuds) na uwasilishe fomu iliyojazwa kwa njia ya faksi, barua au barua pepe (maelezo ya mawasiliano yamechapishwa kwenye fomu) kwa OEO. Faksi: 1-844-886-5196

Wasiliana nasi kuhusu:

Swali au tatizo linalomwathiri mwanafunzi katika shule za umma za K-12 za Washington

Ombi la kupata mafunzo au uhamasishaji katika jamii, shule au mahali pako pa kazi 

Kupata usaidizi kuhusu swali au tatizo lako:

Tafadhali tuwasiliane mtandaoni, au kwa simu, faksi, au barua. Tafadhali kumbuka kuwa ofisi ina wafanyikazi na ufadhili mdogo na inapeana kipaumbele kazi yake kulingana na vigezo vya mpango mkakati / Mpango wa Mikakati.

Utatuzi wa Migogoro Usio Rasmi

Office of the Education Ombuds (OEO) humsaidia mtu yeyote aliye na maswali au hoja kuhusu shule za umma za K-12 za Washington. Tunaweza kukupa maelezo, rufaa, zana na rasilimali nyingine.

Madhumuni ya kisheria ya Office of the Education Ombuds (OEO) ni kupunguza ukosefu wa fursa. Vipaumbele vya mpango wetu wa mikakati hulenga haki ya elimu, hasa kwa jamii zilizoathiriwa sana na COVID-19. Tunatumia rasilimali zetu ndogo za utatuzi wa migogoro, kama vile upatanishi na ukufunzi usio rasmi, kwa wanafunzi wa K-12 ambao:

  • Hawapo shuleni, ikijumuisha wanafunzi wenye ulemavu wanaopokea huduma ya baadhi ya siku za shule
  • Ni watu wa asili ya Kiafrika au wa makabila asili 
  • Hawana makao
  • Wanatunzwa na jamaa au vituo vya makazi 
  • Wanashiriki katika masuala ya haki kwa vijana au mifumo ya kuwarekebisha vijana
  • Ni wahamiaji rasmi au wasio rasmi, wakimbizi, watafutaji makazi rasmi au wanafunzi au familia ambazo lugha yao msingi si Kiingereza au
  • Wanapokea usaidizi wa Mipango ya Wraparound yenye Huduma za Kina (Wraparound with Intensive Services, WISe) au Mipango ya Wagonjwa Wanaolazwa ya Muda Mrefu kwa Watoto (Children’s Long Term Inpatient Programs)

Pata Usaidizi Wetu:

Black and White Icon of electronic device sending message. Created by Priyanka from Noun Project Mtandaoni – Tunakuhimiza utumie Mchakato wetu mpya wa Kujiandikisha Mtandaoni. Utahitaji kufungua akaunti kwa kutumia jina lako na anwani sahihi ya barua pepe. Baada ya kufungua akaunti na kukamilisha mchakato wa kujiandikisha mtandaoni, mtu fulani atawasiliana nawe haraka iwezekanavyo ili kukupa maelezo au kuratibu miadi. Mchakato wetu wa kujiandikisha mtandaoni unapatikana kila wakati, lakini mtu fulani atafuatilia wakati wa saa za kawaida za kazi.

Black and white icon of mobile phone making a call. Created by Thays Malcher from Noun Project.Kwa Simu – Ikiwa unapendelea kuzungumza na mtu ana kwa ana au unahitaji usaidizi wa kukamilisha mchakato wa kujiandikisha mtandaoni, tafadhali tupigie simu kwa nambari ya simu isiyolipishwa 1-866-297-2597 wakati wa saa zetu za kazi za Jumatatu hadi Ijumaa. Wafanyakazi wetu wanaweza kufikia huduma za ukalimani wa simu kwa zaidi ya lugha 150.

Black and white icon of envelope with two papers inside. The first paper has the "at" email icon. The second paper has lines for writing a letter. Created by Anang Taufik from Noun Project.Kwa Faksi au kwa Barua – Pakua fomu ya Kuomba Huduma za Wapelelezi wa Malalamiko ya Wananchi (Ombuds) na uwasilishe fomu iliyojazwa kwa njia ya faksi, barua au barua pepe (maelezo ya mawasiliano yamechapishwa kwenye fomu) kwa OEO. Faksi: 1-844-886-5196

Ikiwa unashirikiana na Wapelelezi wa Malalamiko ya Wananchi (Ombuds) na ungependa kuipa OEO ruhusa ya kujadili hali ya mwanafunzi moja kwa moja na shule na wafanyakazi wa kitengo cha usimamizi wa shule katika eneo jinsi inavyofaa, tafadhali pakua, ujaze na urudishe fomu ya Ruhusa ya Kuwasiliana na Shule.

Ikwia unashirikiana na Wapelelezi wa Malalamiko ya Wananchi (Ombuds), huenda tutahitaji kuangalia rekodi za mwanafunzi wako ili kuelewa matatizo vizuri. Ikiwa tunahitaji kufanya hivyo, basi tutakuomba utupatie ruhusa yako ili shule itoe rekodi. Tunatumia fomu hii kwa utoaji wetu wa rekodi: Ruhusa ya Kutoa Rekodi za Mwanafunzi.

  • Unaweza kuwasilisha fomu hizi kupitia Mchakato wa Kujiandikisha Mtandaoni au kwa faksi, barua au barua pepe.

Tunaweza pia kuwafunza waelimishaji na watetezi wa jamii kuhusu kuwasaidia wanafunzi na kusuluhisha migogoro.

Tafadhali tuma barua pepe kwa oeoinfo@gov.wa.gov au piga simu kwa 1-866-297-2597 ili upate usaidizi huu. Mara nyingi, mmoja wa wahudumu wetu hujibu swali kwa barua pepe au kwa simu. Tunaruhusu mawasiliano kutoka kwa familia, wanafunzi, waelimishaji na wadau wengine wa jamii walio na maswali au matatizo.Ofisi yetu hufanya kazi kwa ushirikiano, kwa njia isiyo rasmi na kwa faragha, ili kuzisaidia familia na shule kusuluhisha migogoro. 

Je, unapaswa kujua nini kutuhusu?

Hati hii fupi inafafanua jinsi Tunavyoshirikiana Na Familia. Tunakuhimiza uisome ili uelewe usaidizi tunaoweza kutoa na ambao hatuwezi kutoa.

Hati hizi zinafafanua jinsi tunavyoweza kuwasaidia waelimishaji na wataalamu wa jamii.