Kuwasiliana Kwa Ufanisi kwa Fasiri

Kadi ya Vidokezo vya Fasiri
Communicating Effectively with Interpretation

Kuwasiliana Kwa Ufanisi kwa Fasiri

 • Schools and districts must provide interpretation when needed to communicate effectively with families who request an interpreter.
 • Shule na wilaya lazima zitoe fasiri panapohitajika ili kuwasiliana kwa ufanisi na familia zinazoomba mkalimani.
 • For interpretation to be effective, everyone involved in the conversation must cooperate and make time for interpretation.
 • Ili fasiri kuweza kufanikiwa, kila mtu anayehusika kwenye mazungumzo ni lazima ashirikiane na kutoa muda wa fasiri.
 • Use this card as needed during an interpreted conversation to receive a complete, accurate and understandable interpretation.
 • Tumia kadi hii inavyohitajika wakati wa mazungumzo ambayo yanafasiriwa ili kupokea fasiri kamili, sahihi na inayoeleweka.
 • Remember, if you do not understand something; ask the person you are talking with to explain. The interpreter can interpret your request for explanation but should not try to answer your questions.
 • Kumbuka, ikiwa huelewi jambo fulani; mwombe mtu unayezungumza naye ili afafanue. Mkalimani anaweza kufasiri ombi lako la ufafanuzi lakini hafai kujaribu kujibu maswali yako.
 • If you believe the interpreter is not interpreting correctly, you can ask to re-schedule with another interpreter.
 • Ikiwa unaamini kuwa mkalimani hatoi fasiri sahihi, unaweza kuomba uli kupanga upya na mkalimani mwingine.
 • Pardon me, I would like to ask…
 • Samahani, ningependa kuuliza...
 • Please pause so the interpreter can tell me what you have said.
 • Tafadhali tulia ili mkalimani aweze kuniambia ulichosema
 • Please repeat that, I am afraid it was not all covered in the interpretation.
 • Tafadhali rudia hiyo, naogopa haikutajwa yote kwenye fasiri.
 • Could we slow down a bit to be sure the interpreter is able to give a full interpretation?
 • Je, tunaweza kuenda polepole kidogo ili kuhakikisha kuwa mkalimani anaweza kutoa fasiri kamili?
 • Could you both repeat what you said, one at a time, so we can be sure the interpreter can cover everything?
 • Je, nyinyi nyote wawili mnaweza kurudia mlichosema, kila mmoja kwa wakati wake, ili tuweze kuhakikisha kuwa mkalimani amepata kila kitu?
 • I do not understand the interpretation very well. Could we try to reschedule with another interpreter?
 • Sifahamu fasiri vizuri. Je, tunaweza kujaribu kupanga na mkalimani mwingine?

Interpretation Support Tips Card Printable PDF

Kadi ya Vidokezo vya Fasiri